Msanii Kanye West aliyekuwa akikabiriwa na kesi ya kumpiga mpiga picha
mwisho mwa wiki iliyopita huko Los Angeles, Marekani, mahakama
imetupilia mbali mashtaka hayo kwa madai ya kwamba hakukua na ushahidi
wa maelezo ya kutosha kuhusu kesi hiyo.
West alitakiwa alipe gharama za kumpiga mpiga picha huyo na kuharibu
kamera ya mpiga picha huyo, hata ivyo Kanye alitamka kuwa yupo tayari
kulipa kiasi chochote cha pesa ikiwa atalazimika kufanya hivyo.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, kinasema Kanye angelazimika kulipa kiasi cha
$ 250,000 kuhusiana na suala hilo....ni mkwanja mrefu japo Kanye
mwenyewe alikuwa tayri kulikamilisha hilo.