Wakati anatolewa BBA, Feza alikiri kumpenda kweli Oneal na alionyesha kabisa anahitaji Oneal awe mwanaume wake wa maisha.
Oneal, Feza and friends
Taarifa ikufikie kwamba Feza ambae ni mama wa mtoto mmoja, ameshafika Botswana na kupokelewa kwa shwangwe na Mawifi na Mashemeji waliojitokeza kuanzia uwanja wa ndege.
I'm still overwhelmed by Batswana. I'm in shock, I don't know what I did yo. I'm speechless. I thank you & ke a le rata.
— Feza Kessy (@FezaKessy) August 21, 2013
Kama hiyo haitoshi, Feza ameonekana kuwa na furaha kupitiliza... ametumia page yake ya twitter kueleza sehemu ya hisia zake juu ya mapokezi na mpenzi wake Oneal.
Mapokezi mazuri hayajaonekana Airport tu au barabarani bali mpaka kwenye mtandao wa twitter ambako Wabotswana wengi wamefurahishwa na muunganiko wa wawili hao ambao mapenzi yao yameanzia kwenye shindano la BBA 2013 walikokutana kwa mara ya kwanza.
Motamma, Feza and Oneal
Oneal na Feza watajumuika na mashabiki wao kwenye chakula jioni kwenye Oneza Gala Dinner 22 August, ambapo kila shabiki atakaeingia atalipia kiingilio.
Je Feza ndio amekwenda Botswana moja kwa moja? Itakua kama Elizabeth Gupta ambae kaolewa na Kevin wa Nigeria? Endelea kupita hapa kuna interview inakuja.
RT @OnealBBA: THE TICKET FOR ONEZA'S GALA DINNER AT GRANDPALM HOTEL TOMORROW. pic.twitter.com/JUhr15fovw
— Oneal™ (@Onizee) August 21, 2013