Diamond Platnumz jana alifanya uzinduzi wa video ya wimbo wake mpya, Number 1 kwenye ukumbi wa Serena Hotel jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo ulihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo ndugu zake, marafiki, wasanii wenzake na wadau mbalimbali wa muziki nchini.
Chege Chigunda akifuatilia kwa makini
Kwenye uzinduzi huo pia, Diamond alimpa zawadi ya gari msanii mkongwe aliyetangaza kustaafu muziki, Muhidin Gurumo kama heshima kwake.
Diamond akienda kumkabidhi Mzee Muhidin Gurumo gari
Diamond akimuonyesha Mzee Gurumo gari aliyomzawadia
Diamond akiongea na wadau waliofika
Dully Sykes akiwa na Diamond wakiongea machache
Ndugu na Marafiki katika picha ya pamoja
Hapa Diamond akimkabidhi Mzee Gurumo funguo ya gari
Diamond akiongea machache na wasanii wenzake waliofika kumpa sapoti
Hili ndo gari alilopewa Mzee Gurumo na Diamond
Hivyo ndivyo watu walivyojitokeza kuja kuona video ya Number 1
Kama kawa burudani ilikuwepo kidogo
Mzee Gurumo akijaribu kidogo kupiga lesi baada ya kukabidhiwa gari
Mzee Gurumo akiongea machache na kumshukuru Diamond kwa kumpatia zawadi ya gari
Nay wa Mitego akiwa pamoja na Madam Rita
Queen Darleen na Bi Sandra
Ray Kigosi akifuatilia kwa makini sana
Wadau mbalimbali waliopata mualiko wakifuatilia
Wadau wa burudani wakifuatilia
Wadau wakisubiri kwa hamu kuona kuona video ya Number 1
Watu wakifuatilia
Asha Baraka,Queen Darleen pamoja na Mama Diamond
c