Msanii wa Orijino Komedi Lucas Mhuvile 'Joti' (katikati), akishuhudia uzinduzi huo na marafiki zake.
Baadhi ya mashabiki walihudhuria kwenye uzinduzi huo wakifuatilia kwa makini.
MSANII
wa Filamu Bongo, Elizabeth Michael 'Lulu', usiku wa kuamkia leo
amefanikisha zoezi la uzinduzi wa filamu yake mpya inayokwenda kwa jina
la Foolish Age Tukio la uzinduzi huo lilifanyika katika Ukumbi wa
Mlimani City jijini Dar, na kuhudhuriwa na mastaa kibao wa tasnia
mbalimbali hapa Bongo, wakiwemo; Judith Wambura 'Lady Jaydee', ambaye
alitumbuiza sambamba na Barnaba na Amini.