Jumanne (August 20) tiketi za mashindano hayo makubwa duniani zilianza kuuzwa kupitia mtandao wa shirikisho la soka duniani FIFA na kwa mujibu wa BBC, FIFA imesema kuwa zaidi ya tiketi milioni moja zimeombwa kupitia mtandao wake ndani ya saa saba pekee tangu zianze kuuzwa.
Wengi walioagiza tiketi hizo ni mashabiki kutoka Brazil, Argentina, Marekani na Uingereza. Mechi za ufunguzi zitafanyika Alhamisi (June 12) na fainali itafanyika Jumapili (July 13) mwakani.
Mashabiki wa soka wanaweza kuomba tiketi hizo kupitia mtandao wa FIFA hadi tarehe kumi Oktoba.