Siku mbili zilizopita Huddah Monroe alitweet kusema kuwa hataweza kuhudhuria fainali za Big Brother ‘The Chase’ itakayofanyika Jumapili hii nchini Afrika Kusini kutokana na sababu zisizozuilika.
Taarifa hiyo ilionekana kuwasikitisha mashabiki wake wengi ambao walikuwa na shauku ya kumuona mshiriki huyo wa Kenya kwa mara nyingine kupitia camera za DSTV kwa mara ya mwisho kwenye The Chase.
HUddah na Annabel
Wote tukiwa tumeshaamini kuwa Boss Lady hatakuwepo katika fainali hizo, leo Huddah ametu-surprise kwa kupost picha akiwa na mshiriki mwenzake wa ‘The Chase’ Annabel na kuandika “With Annabel heading to SOUTH AFRICA…..JOBURG’ we comin baby…….large up urselves!”
Pia masaa matatu yaliyopita Annabel naye alitweet “Off to SA with my girl @HUDDAHMONROE woop! Woop!”.
Hii inamaanisha zile sababu zilizokuwa nje ya uwezo wa Huddah kumsababisha kushindwa kwenda Afrika Kusini kama alivyokuwa amesema zimetatuliwa, au nashawishika kuamini kuwa tweet yake ya juzi ya kutohudhuria fainali hizo huenda alitaka kuona kiasi gani watu watasikitika kusikia habari hiyo!!
Post Top Ad
Your Ad Spot
Friday, August 23, 2013
Home
Unlabelled
HUDDAH NA ANABEL WAELEKEA NCHINI AFRICA KUSINI KWENYE FAINALI ZA BIG BROTHER, BAADA YA HUDA KUSEMA HATAHUDHURIA.
HUDDAH NA ANABEL WAELEKEA NCHINI AFRICA KUSINI KWENYE FAINALI ZA BIG BROTHER, BAADA YA HUDA KUSEMA HATAHUDHURIA.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.