Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, October 22, 2013

HUYU NDIYE MSANII WA GOSPEL NCHINI UGANDA ALIYEFARIKI KATIKA SWIMMING POOL JIJINI DAR ES SALAAM

Msanii wa gospel wa nchini Uganda, Mutalya Elvis maarufu kama Mac Elvis amefariki dunia. Msanii huyo alifariki kwa kuzama kwenye bwawa la kuogelea nchini Tanzania ambako alikuja na wasanii wengine wa Uganda waliokuwa kwenye ziara ya shule na makanisa.
3939472
Mwili wa msanii huyo ulipatikana ukielea kwenye bwawa hilo la kuogelea. Mac ni msanii mkubwa mno wa gospel nchini Uganda na pamoja na kuimba, alikuwa mtayarishaji wa muziki na mhubiri pia.
Elvis alilelewa kwenye kituo cha Watoto Child Care baada ya kuchukuliwa alipokuwa na miaka 6 kutokana na kufiwa na wazazi wake.
“Sad News has just hit me that Ugandan Gospel singer Mac Elvis has died, this is so terrible! Such a talented loving young man,may his soul rest in peace,”aliandika msanii wa Uganda Maurice Kirya.
RIP Elvis

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages