NI ukatili uliopitiliza! Hausigeli aliyejulikana kwa jina moja la
Ester (14) yupo matatani kwa madai ya kumuua mtoto Arafat Allan (3) kwa
kumnyonga shingo na kumpiga na kitu kizito kichwani kisha kuutumbukiza
mwili wake kwenye dimbwi la maji machafu, Risasi Jumamosi limekamata
tukio zima.
Tukio hilo lilijiri Jumapili iliyopita Mailimoja, Kibaha mkoani Pwani ambako marehemu alikuwa akiishi na wazazi wake.
Akizungumza kwa uchungu, mama mzazi wa mtoto huyo, Zakia Peter ambaye
amelazwa katika Zahanati ya Kellen kutokana na mshtuko wa kifo cha
mwanaye, alisema siku ya tukio, hausigeli huyo aliyekuwa na siku mbili
tangu aanze kazi aling’ang’ania kutumwa sokoni saa mbili asubuhi ambapo
alimkubalia na kumuagiza mboga.
AONDOKA NA MTOTO
Bila mwanamke huyo kujua, msichana huyo alimpitia Arafat kwa jirani
alikokuwa akicheza na wenzake na kuondoka naye kwa madai anamsindikiza.
“Nilipoona muda unasonga mbele bila hausigeli kurudi na mtoto nilianza kuwatafuta,” alisema mama wa marehemu.
Akasema aliwatafuta kwa muda mrefu bila mafanikio mwishowe yeye na
majirani zake wakaenda kutoa taarifa polisi na kufunguliwa jalada la
kesi KB/RB/1154/2013 TAARIFA.
HABARI ZASAMBAA MAITI YA MTOTO KUONEKANA KWENYE DIMBWI LA MAJI
Mama wa marehemu aliendelea kusema kuwa zoezi la kumsaka msichana huyo
na mtoto wake liliendelea mpaka Jumanne iliyopita ambapo habari
zilisambaa kwamba kuna maiti ya mtoto wa kiume imekutwa ikielea kwenye
dimbwi la maji machafu linalotumika kumwagilia bustani za mboga maeneo
hayo.
“Niliondoka na ndugu wengine hadi kwenye dimbwi hilo! Nilipata
mshtuko mkubwa kukuta maiti ya mtoto anayeelea ni ya mwanangu Arafat,”
alisema huku machozi yakimtoka.
MADAKTARI WAANIKA RIPOTI YA UCHUNGUZI
Baada ya hapo, mwili huo
ulipelekwa katika Hospitali Teule ya Tumbi, Kibaha ambapo madaktari
waliufanyia uchunguzi na kubaini kuwa marehemu alinyongwa shingo na
kupigwa na kitu kizito kichwani hali iliyomsababishia mauti.
MAUAJI YAHUSISHWA NA USHIRIKINA
Baadhi ya watu waliozungumza na
gazeti hili Jumatano iliyopita akiwemo mama wa marehemu, walisema kwa
siku mbili hizo alizofanya kazi hausigeli huyo alionekana kuwa na mambo
ya kishirikina kwani asubuhi ya siku ya tukio aliamka akiwa amenyolewa
nywele upande mmoja.
“Siku hiyo ya Jumapili huyo mdada wa kazi
aliamka akiwa amenyolewa nywele upande mmoja, alipoambiwa amalizie zote
alikataa akisema atanyoa baada ya kutoka sokoni ambapo hakurudi tena,”
alisema mama wa marehemu.
HAUSIGELI AKAMATWA
Jumatatu iliyopita, siku moja baada ya tukio,
hausigeli huyo alikutwa akirandaranda stendi akiomba fedha za nauli ili
arudi kwao Mbeya lakini alikamatwa na kufikishwa kwenye kituo kidogo cha
polisi.
Habari zinasema hali kwenye kituo hicho ilikuwa mbaya
kufuatia baadhi ya wakazi wa eneo hilo kujaribu kukivamia ili wamuue
mtuhumiwa huyo. Ilibidi mtuhumiwa ahamishiwe Kituo cha Polisi cha Tumbi,
Kibaha.
MANENO YA WATU WA KARIBU
Kwa mujibu wa watu wa karibu wa familia
hiyo, msichana huyo aliokotwa na ndugu wa baba wa marehemu baada ya
kumkuta barabarani akiomba msaada akidai anateswa na ndugu zake,
wakampeleka kwa baba wa marehemu ili wamsaidie ambapo walimpa shughuli
ya kazi za ndani.
Baba wa marehemu, Allan hakuweza kuzungumza
kutokana na kuwa kwenye hali mbaya katika Zahanati ya Kellen alikolazwa
baada ya mwanaye kuzikwa katika Makaburi ya Mailimoja, Jumatano
iliyopita.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Saturday, October 12, 2013
Home
Unlabelled
HUYU NDIYE MTOTO ALIYENYONGWA NA HOUSEGIRL
HUYU NDIYE MTOTO ALIYENYONGWA NA HOUSEGIRL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment