Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, October 8, 2013

KALA JEREMIAH ATANGAZA KUMZAWADIA MTU ATAKAYESAIDIA KUREJEA KWA PAGE YAKE YA FACEBOOK ILIYOIBIWA

Likes kwenye akaunti za Facebook zimegeuka kuwa kama mtaji mkubwa kwa makampuni mengi duniani. Makampuni hayo yako radhi kulipa mabilioni ya dola kujitangaza tu mtandaoni kwa kampeni za kutafuta likes za Facebook. Hii ni kwasababu, kama kampuni likiwa na likes nyingi kwenye ukurasa wake, inakuwa rahisi kufikisha ujumbe kwa haraka bila gharama yoyote.

Ona hata Tanzania jinsi makampuni ya simu, makampuni ya bia na mengine yalivyoweka nguvu kutafuta watu zaidi watakaobonyeza kile kitufe cha ‘Like’. Na hata watu maarufu pia, likes zimegeuka mtaji mkubwa kwao ambapo wengi wanaozipenda kurasa zao ni mashabiki. Hivyo, kwa mtu kama Kala Jeremiah ambaye mpaka sasa ukurasa wake wa Facebook umefikisha zaidi ya likes 52,000, kuipoteza si jambo la kawaida.
1234490_227425904086760_1116039448_n
“Wameihack na wanapost vitu vyao wanapost vitu vyao wanavyotaka. Jana wamepost tangazo la mikopo, mimi nikajaribu kucomment na nikawaambia watu kwamba sio kweli. Nawaambia watu kuwa ile sio page yangu tena nimefungua page mpya inaitwa Kala0444. Hii page ya Kala Jeremiah ‘imeibiwa’ na siitumii tena,” Kala aliiambia Bomba FM jana.
Bongo5 imeongea pia na Kala ambaye amesema imemuuma kwa kiasi kikubwa kuipoteza akaunti aliyokuwa ameijenga hadi hapo ilipofika na atapambana hadi irejee kawaida. Amesema akaunti yake ilikuwa ikimweka karibu na mashabiki wake popote pale alipokuwa akitembea, na anahisi mipango yake haipo salama tena kwakuwa kuna jumbe za muhimu na biashara zimo kwenye inbox yake, hivyo ana wasiwasi kuwa atatapeliwa.
Ameimbia Bongo5 kuwa, kuna watu wanaomsaidia kwa sasa kuwasiliana moja kwa moja na makao makuu ya Facebook ili kupata utatuzi wa suala hilo na amesema kama kuna mtu atakayeweza kumsaidia kuikomboa akaunti hiyo atamzawadia.
Kala si msanii wa kwanza kupatwa na mkasa huo, akaunti za Diamond na Lady Jaydee zimewahi kuingiliwa na hackers na wakawa wanapost mambo ya mikopo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages