Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, October 18, 2013

MRISHO MPOTO ATANGAZA OFA KWA WEZI WALIOIBA VIFAA VYA GARI LAKE KUVINUNUA KWA SHILINGI MIL 2 KUTOKA KWAO

Mrisho Mpoto aka mjomba ametangaza ‘fursa kwa wezi’ ambao usiku wa kuamkia Jumatano wiki hii walimuibia vifaa vya gari lake jipya ambalo amedai kuwa hana muda mrefu nalo.


Mpoto amedai kuwa mbali na vifaa vya gari lake ambavyo vimeibiwa na wezi hao pia kuna vitu vingine muhimu vikiwemo vitabu vyake, hivyo amewasihi wezi hao wamrudishie vitu hivyo.
BWtilJCCIAITSgi
Kupitia ‘You Heard’ ya XXL leo Mjomba ametangaza ofa kwa yeyote aliyehusika kumuibia amrudishie vitu vyake na kuongeza kuwa yuko tayari kuvinunua kutoka kwa wezi hao kiasi kisichozidi shilingi 2,000,000.

“natumia fursa hii au nafasi hii kuwaomba mnirudishie aidha kwa kunionea huruma kama mjomba, lakini pia niko tayari kulipia na kiasi ambacho naweza nikaahidi kulipia kwa mtu ambaye ataweza kunirudishia vitu vyangu ni thamani ya shilingi milioni mbili niko tayari kurudisha, kwahiyo wezi mlioiba vitu vya mjomba naomba mnirudishie tafadhali”.
Alisema mjomba Mrisho Mpoto.
Haya kazi kwenu wezi!!

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages