INGAWAJE Said (38), mkazi wa Bagamoyo kwa Mtoro, Pwani ambaye aliteseka na uvimbe mkubwa usoni kwa miaka 12 sasa amepona baada ya kufanyiwa upasuaji katika Hospital ya CCBRT iliyopo jijini Dar.
Ngawaje alisema matunda hayo ameyapata baada ya gazeti hili la Machi 11, mwaka huu kutoa habari yake ukurasa wa 15 akielezea matatizo yake, watu mbalimbali walimchangia fedha kwa ajili ya matibabu.
“Halafu akajitokeza mfadhili mmoja ambaye alitoa fedha zote za kufanyiwa upasuaji ambapo upasuaji wa kwanza alifanyika Julai 15, mwaka huu na wa pili Oktoba 30, mwaka huu.
“Kwa sasa hata kuoa naweza maana huko nyuma hakuna mwanamke aliyekuwa akinipenda kutokana na tatizo nililokuwa nalo, nawashukuru sana watu wa Gazeti la Uwazi kwa kutoa habari yangu na watu kunisaidia, kwa kweli nimemuona Mungu,” alisema Ngawaje.
No comments:
Post a Comment