Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, October 27, 2012

PADRI ALIYEFUNGISHA NDOA YA UWOYA AFARIKI DUNIA


MCHEZA filamu mkali Bongo, Irene Uwoya au mama Krish, amepata pigo baada ya kufiwa na padre aliyewafungisha ndoa yeye na Hamad ‘Kataut’ Ndikumana katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Dar es salaam mwaka 2009.

Marehemu, mbali na kuwa padri pia alikuwa baba mkubwa wa Uwoya na katika utumishi wake wa kiroho alikuwa mkoani  Kilimanjaro.

 “Yule aliyewafungisha ndoa ni baba yake mkubwa na alikuja tu mara moja Dar kwa ajili ya shughuli hiyo kwa vile yeye ni padre, alifariki dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi,” alisema mtoa habari wetu.
 
Uwoya akimvisha pete Ndikumana siku ya ndoa yao.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages