KATIBU wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda, na wenzake 49 leo wamepandishwa kizimbani kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam na kusomewa mashitaka manne ya kufanya vurugu kwa kuvamia kiwanja kilichopo Chang’ombe jijini Dar es Salaam ambacho ni mali ya Agritanz.
Sheikh Issa Ponda na wenzake wakiwasili mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
Kesi hiyo yenye namba CC 240, shitaka la
kwanza ni kula njama za kutenda kosa, shitaka la pili ni kuingia kwa
nguvu eneo ambalo hawaruhusiwi, shitaka la tatu ni kujimilikisha ardhi
kinyume cha sheria na kosa la nne ni wizi.
Washitakiwa wote wamekana mashitaka na kupelekwa mahabusu mpaka Novemba Mosi mwaka huu kesi itakapotajwa tena mahakamani hapo.
Washitakiwa wote wamekana mashitaka na kupelekwa mahabusu mpaka Novemba Mosi mwaka huu kesi itakapotajwa tena mahakamani hapo.
Sheikh Ponda akishuka kwenye gari eneo la mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar.
Baadhi ya washitakiwa katika kesi hiyo nao wakielekea mahakamani leo.
Watuhumiwa wakiwa chini ya ulinzi kabla ya kuingia mahakamani.
Sheikh Ponda na watuhumiwa wenzake wakiwa ndani ya mahakama kusikiliza kesi yao.
Wanahabari wakichukua picha za matukio ndani ya mahakama.
Sheikh Ponda akiongea na mwanasheria wao, Juma Nassoro kabla ya kesi kuanza kusikilizwa.
Watuhumiwa wakirudishwa kwenye karandinga baada ya kesi yao kuhairishwa mpaka Novemba Mosi mwaka huu itakapotajwa tena.
Sheikh Ponda akipandishwa kwenye karandinga baada ya kesi hiyo.
Ulinzi ulivyokuwa umeimarishwa eneo la mahakama.
No comments:
Post a Comment