Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, October 24, 2012

WOMEN IN BALANCE, KITCHEN PARTY GALA YAWAPA ELIMU UNYUMBA WANAWAKE JIJINI DAR.


Msemaji katika Hafla ya Women in Balance Kitchen Party Gala Mhadhiri Msaidizi wa Idara ya Saikolojia katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bw. Chris Mauki akitoa somo la Saikolojia kwa wakinamama na wasichana waliohudhuria hafla hilo iliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee VIP Hall jijini Dar.
Life Style Designer of Sex and Relationships kutoka Kenya Bi. Getrude Mungai akitoa somo la kuhusiana na masuala ya mahusiano ya kimapenzi kwa wenye ndoa na wasiokuwa na ndoa ambapo amesema vipo vitu vingi vinavyochangia kuboresha ama kuharibu mahusiano hayo ambapo wahusika wanatakiwa kuvifahamu na kuvitilia mkazo ili kudumisha mahusiano yao.
Mafunzo kwa vitendo yalihusika pia.
Msemaji wa mwisho alikuwa ni Mama Veronica aliyewaacha hoi kwa vicheko wanawake waliohudhuria Kitchen Party Gala ambapo alizungumzia masuala ya uvumilivu katika ndoa sio tu kukosekana kwa kipato ndani ya nyumba bali hata mikimiki ya Unyumba kwa wanandoa.
Independent Sales Consultant wa bidhaa za Oriflame Bi. Jesca Mwakyulu akionyesha bidhaa ya Feminele Intimate Wash ya Oriflame ambayo ameisifia kuwa na Natural Lactic Acid ambayo inasaidia kutunza hali halisi ya sehemu za siri za Mwanamke.
Amefafanua kuwa kwa asili sehemu hizo zina hiyo Lactic Acid ambayo hutunza unyevu sahihi na Bacteria wazuri ambao husaidi kutoa ulinzi dhidi ya Fangasi, miwasho na harufu mbaya.
Mmoja wa wadhamini wa Women in Balance Kitchen Part Gala Mwakilishi kutoka TSN Super Market Lizbeth akitangaza zawadi kumi kwa wageni waliohudhuria Kitchen Party Gala zikiwemo Vocha za kufanya Shopping katika Super Market za TSN zilizopo jijini Dar es Salaam.
Wakinadada wakionekana kufurahishwa na mambo yaliyokuwa yakizungumziwa kwenye Kitchen Party Gala hiyo.
Mkurugenzi wa Prime Time Promotions, Juhyna Kusaga (kushoto) na mdogo wake.
Kwa picha zaidi bofya read more

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages