Akiwa Serengeti, JT na mke wake aliyefunga naye ndoa iliyogharimu dola
milioni 6.5 alifikia katika hifadhi ya Singita Grumeti yenye hoteli bora
na za kifahari duniani. Gharama ya hoteli hizo kwa usiku mmoja ni
sababu kubwa ya kwanini watanzania wengi si tu washindwa kwenda angalau
kupumzika kwa usiku mmoja, hawaifahamu kabisa.
Usiku mmoja pale inabidi uingie kwenye akaunti yako na unyofoe $5,700
ambazo kwa madafu shilingi ya Tanzania ni kama milioni 9 hivi! Duuh! Cha
kushangaza zaidi ni kuwa gharama hiyo hutozwa kwenye msimu ambao hauna
watalii wengi yaani "low" season otherwise ingemgharimu JT $7,620 kwa
usiku mmoja (zaidi ya shilingi milioni 11) katika kiota cha Sasakwa
Lodge ili kupata kile kinachoitwa ‘ private villa retreat.’
Sasakwa Lodge
Mume huyo mpya na mke wake waliwasili Tanzania siku mbili baada ya ndoa
yao ya October 19 na kuonekana kwenye picha zilizopigwa kwa mbali
wakishuka kutoka kwenye ndege.
No comments:
Post a Comment