Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, November 6, 2012

HIVI NDIVYO WAMEREKANI WANAVYO ENDELEA KUPIGA KURA



 
 
vituo vya kupiga kura vimefunguliwa leo na tayari wananchi wa Marekani wameanza kupiga kura kuchagua rais atakayewaongoza tena huku kukiwa na ushindani mkali kati ya Barack Oboma na mgombea urais wa  chama cha Republican, Mitt Romney.

Kampeni za urais mwaka huu zimegharimu fedha nyingi zaidi kuliko kampeni nyingine katika historia za uchaguzi wa Marekani.

Rais Obama alitoa wito wa mwisho kwa wapiga kura katika mkutano wa kisiasa uliofanyika katika Jimbo la Lowa akiwataka wananchi wa Marekani wampigie kura.
Ushindani mkali

Ushindani katika uchaguzi huu ni mkali sana na mpinzani wa Rais Obama wa chama cha Republican Mitt Romney ambaye amekuwa akipita kwenye majimbo mawili makuu Ohio na Pennsylvania mara kwa mara.

Katika baadhi ya majimbo Obama amekuwa akiongoza, lakini kwa tofauti ndogo huku katika mengine wakifungana yaani kupata kura sawa.

Kura ya mwisho ya kutafuta maoni iliashiria kuwa rais Obama anaongoza katika majimbo mengi ambayo wagombea wote wana nafasi ya kushinda.

Lakini kura hiyo inaashiria pia huenda idadi ya watu watakaojitokeza kupiga kura ikawa kubwa kwa Romney.

Kura za kwanza zilipigwa katika eneo la Dixville Notch katika Jimbo la New Hampshire  na wagombea wote walitoka sare.

Kampeni za aina yake

Wakati wananchi wa Marekani wakiendelea kupiga kura Romney alikuwa akiendela kufanya kampeni huku mpinzani wake, Obama akifanya kampeni ya aina yake, ya kuwapigia simu wapiga kura na kuwatembelea.

Pia Obama alionekana katika lininga ya CNN akisalimia wapiga kura huku akisaini kiatu cha mpiga kura mmoja. Wachunguzi wa masuala ya kisiasa wanasema Romney atapata kura nyingi kutoka katika vyuo vikuu.

Historia za wagombea wa urais, Barack Obama na Mitt Romney

Baraka Obama atetea kiti cha urais

Barack Obama alichaguliwa kuwa Rais wa 44 wa Marekani Novemba 4, 2008 na kuweka historia kwa kuwa Rais wa kwanza mwenye asili ya Afrika. Aliapishwa katika Ikulu ya Marekani Januari 20, 2009.

Alitunukiwa Tuzo ya Nobel Oktoba 9,2009 kutokana na jitihada za kutafuta suluhu katika mzozo wa Mashariki ya Kati.

Alichaguliwa kwa mara kwanza kuwa Seneta wa Jimbo la Illinois Novemba 2, 2004 na baadaye kujipatia umaarufu mkubwa kwenye majukwaa ya kisiasa.

Obama alitangaza dhamira ya kuwania urais kwa mara ya kwanza Februari 10, 2007 na mwaka uliofuata alitimiza ndoto yake.

 Kumbukumbu zinaonyesha kwamba Obama alianza kupata umaarufu katika majukwaa ya kimataifa mwaka 2004 wakati alipokaribishwa kwenye kongamano la Chama cha Democrat kwa ajili ya kutoa hotuba ya utangulizi.

Obama ni Mwanasheria amepata Shahada ya Uzamivu (Phd) na kubobea kwenye maeneo ya  katiba na haki za kiraia.

Alizaliwa Agosti 4, 1961 Honolulu, Hawai na kupata shahada yake ya kwanza ya Uhusiano wa Kimataifa mwaka 1983 katika Chuo Kikuu Columbia. Baadaye alisoma sheria katika Chuo Kikuu cha Havard na kufanikiwa kuwa mhakiki wa kwanza mweusi aliyejumuishwa kwenye jopo la mapitio ya katiba.

Alioana na Michele Robinson Octoba 18, 1992 na wote wawili wamefanikiwa kupata mabinti wawili Malia na Sasha.

Mgombea wa urais, Mitt Romney

Willard Mitt Romney, anapeperusha bendera ya Chama cha Republican baada ya kushindwa katika jaribio lake dhidi John ya McCain katika kinyang’anyiro cha mwaka 2008.

Alianza kupata umashuhuri wa kisiasa tangu mwanzoni mwa miaka ya 1990, wakati alipojaribu bila mafanikio kumwangusha mgombea wa Democrat, Ted Kennedy kwenye uchaguzi wa seneti wa mwaka 1994.

Romney ambaye ni Gavana wa zamani wa jimbo la Massachusetts ni mtoto wa Gavana wa zamani wa Jimbo la Michigan. Kwa hivi sasa ni mfanyabiashara mkubwa akidhaniwa kumiliki makampuni kadhaa ambayo yamesambaa pia katika nchi za Mashariki ya mbali.

Alihitimu shahada za zake katika fani za sheria na biashara katika Chuo Kikuu cha Havard mwaka 1969.

Alizaliwa Machi 12,1947, Michigan
Mwaka 2003 alichaguliwa Gavana wa 70 wa Jimbo la Massachusetts na kutumikia nafasi hiyo katika kipindi cha muhula mmoja.

Familia yake ina historia ya kujihusisha na masuala ya siasa. Baba yake mzazi George Roomney aliwahi  kuingia kwenye kinyang’anyiro cha urais mwaka 1968.

Mwaka 2010 aliandika kitabu alichokiita “hakuna kuomba radhi.” Ameoana na Davies na wote wawili wamefanikiwa kupata watoto watano.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages