WANAHARAKATI
nchini China wanasema kuwa vijana watatu watawa wa Tibet pamoja na mama
mmoja walijiteketeza mkesha wa kongamano la chama cha tawala cha
kikomunisti nchini China.
Shrika
la Free Tibet linasema kuwa mmoja wa watawa hao alifariki katika kile
inachosema ni idadi kubwa ya watu kujiteketeza kama njia ya kuonyesha
kukerwa na utawala wa china.
Matukio
ya hivi karibuni ya watu kujiteketeza moto katika maeneo ya china
yaliyo na watu wa Tibet yamefikisha idadi ya watu hao wanaojiteketeza
kuwa zaidi ya watu sitini tangu mwaka jana.
Wengi wao wamefariki. Na huenda kuna umuhimu katika wakati ambapo visa hivi vimetokea.
Kuimarishwa
kwa usalama kote China kwa kongamano la chama tawala cha kikomyunisti
nchini, hakujazuia malalamiko ya raia wa Tibet dhidi ya utawala wa
China. Badala yake yameongezeka.
Wanaharakati wanasema idadi ya watu kujiteketeza kwa muda wa siku moja, hii leo, haikutarajiwa.
Tangu
mwaka jana zaidi ya raia sitini wa Tibet wameamua kutumia njia kubwa
kabisa ya kuonyesha kuvunjwa moyo, kwa kile wanachosema ni ukandamizaji
wa China kwa tamaduni zao.
Maafisa
wa serikali wa China wametoa fedha katika maeneo yaliyo na raia wa
Tibet na wameendelea kukana tuhuma hizo za ukandamizaji.
Mkurugenzi
wa kundi linalotetea kuachiwa huru maeneo ya Tibet, amesema malalamiko
ya hivi karibuni yananuiwa kutoa ishara kwa kizazi kipya cha uongozi
China, kitakachoidhinishwa katika kongamano linaloendelea Beijing, kuwa
raia wa Tibet wataendelea kupigania uhuru wao.
Baadhi
ya raia wa Tibet walio uhamishoni, wanatumai kuwa mwanamume
anayedokezwa kuwa kiongozi mpya, Xi Jinping, huenda akawapatia nafasi ya
kufanyika mabadiliko.
No comments:
Post a Comment