Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, December 21, 2012

TASWIRA MBALIMBALI KATIKA USHINDI WA GODBLESS LEMA LEO



Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema) Godbless Lema (wa tatu kushoto) akiwa pamoja na Mbunge wa Jimbo la Ubungo (Chadema), John Mnyika (wa pili kushoto)  wakielekea makao makuu ya chama  hicho baada ya ushindi wa rufaa ya Lema leo jijini Dar.
Sehemu ya nyomi ya wapenzi wa Chadema waliojitokeza kusherehekea ushindi huo.
...Safari ya kuelekea Kinondoni makao makuu.
Wapenzi wa Chadema wakisherehekea ushindi wa Lema jijini Dar leo.
Godbless Lema akiongea na wanahabari baada ya kushinda rufaa ya kesi yake.
Msafara wa wana-Chadema ukielekea makao makuu Kinondoni.
Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe akihojiwa kuhusiana na hukumu ya rufaa hiyo.
Wanahabari pamoja na wapenzi wa Chadema wakiwa makao makuu ya chama hicho Kinondoni.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt. Willbroad Slaa akiongea na wanahabari.
Mama huyu naye hakuwa nyuma kusherehekea ushindi wa Lema
Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) akiwasili katika makao makuu ya chama hicho.
Aliyekuwa wakili wa Lema, Tundu Lissu akielezea jinsi kesi hiyo ilivyokuwa.
Waandishi wa habari wakiwa katika harakati za kupata habari.
...Shamra shamra zikiendelea baada ya ushindi wa rufani hiyo.
Mahakama ya Rufaa Tanzania ambapo kesi ya Lema imetolewa hukumu leo.
---
MAHAKAMA ya Rufaa Tanzania, leo imetoa  hukumu ya rufaa ya kesi iliyokuwa inamkabili aliyekuwa Mbunge wa Arusha  Mjini kwa tiketi ya Chadema, Godbless Lema, ambapo imemrudishia kiti hicho cha Ubunge. Mahakama imejiridhisha kuwa madai ya udhalilishaji hayakuathiri uchaguzi wala mlalamikaji. Walalamikaji wameamriwa kulipa gharama za kesi hiyo tangu ilipofunguliwa mpaka ilipoishia.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages