Ili kuondokana na giza na baridi katika kipindi cha msimu wa ‘winter’ halmashauri ya mji huo imetumia zaidi ya pesa ya Norway kronor milioni 5 (zaidi ya billioni 1) kuweka vioo tatu vikubwa ‘heliostats’ vilivyotegeshwa juu ya bonde ikiwa ni mita 450 juu ya mji vitakavyomulika jua halisi na kumulika katika mji huo.
Helikopta zitatumika kufunga vioo hivyo na zitakuwa zikifuatilia mwenendo wa jua na kumulika mwanga moja kwa moja katika ‘main square’ ya mji wa Rjukan ili kuwasaidia wakazi wa mji huo mdogo ambao wamekuwa wakifunga safari kila mwaka kwenda juu ya mlima mrefu ili kupata joto la jua halisi.
Tazama jinsi helikopta zitakavyokuwa zikifanya zoezi hilo la kuzungusha vioo vya kumulika jua katika mji huo