Inadaiwa kuwa siku ya Alhamisi asubuhi (August 1) kituo cha TV cha BBC kilirusha video ya wimbo “I Could Have Married Kate” ya kikundi cha muziki cha Comedy kiitwacho ‘Barbershopera’ bila wao kugundua katika video hiyo kuna picha inayomdhalilisha Prince William iliyochorwa nyeti za mwanaume katika uso wake.
Watazamaji ndio waligundua picha hiyo na kuanza kutweet kuhusiana na walichokiona.
Baadae BBC waliomba radhi kwa kusema ‘Barbershopera’ waliwaletea video hiyo na kwa bahati mbaya maproducer wao hawakugundua kasoro hizo mapema.
“the material was provided by Barbershopera but we failed to spot the offending material within it. We apologize for this.” BBC waliomba radhi mchana wa siku hiyo.
Tazama video hiyo