Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, August 14, 2013

MSANII BONGO MOVIE ACHOMWA KISU USONI.

Na Imelda Mtema
MSANII wa filamu Bongo, Hamisa Moshi (pichani) hivi karibuni amechomwa kisu usoni akiwa maeneo ya nyumbani kwao Ilala, Bungoni jijini Dar huku akiwahusisha wasanii wenzake na unyama huo.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, Hamisa alisema siku ya tukio alipigiwa simu na kijana aitwaye John akimtaka wakutane ili wazungumzie dili la kazi.
“Aliponipigia simu akaniambia tukutane, tukakutana maeneo ya Ilala. Yeye alikuwa kwenye gari, akaniambia niingie. Kwa hofu nikasita, mara likaja gari likiwa na wasichana watatu ambao walinianzishia vurugu na mmoja akanichoma kisu.

“Nilipiga kelele za mwizi ndipo watu walipokuja na kutaka kuwapiga wakidhani ni wezi, nikawazuia ila nakawaambia tuwapeleke polisi ambako niliwafungulia jalada la kesi lenye namba ILA/RB/2952/2013 KUJERUHI.
“Baada ya hapo nilipewa PF3 kabla ya kwenda Hospitali ya Amana na kushonwa nyuzi nane,” alisema Hamisa.
Hata hivyo, msanii huyo alishangazwa na maelezo yaliyotolewa polisi na watuhumiwa hao waliotajwa kwa majina ya Merry, Tiko, Thecla na Mile kwamba eti walikuwa wakimdai shilingi milioni moja, kitu ambacho si kweli.

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages