Mkurugenzi
wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bi. Kushilla Thomas
akimkabidhi Rais Jakaya Kikwete jezi iliyosainiwa na wachezaji wote wa
timu ya FC Barcelona Ikulu jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni kutambua
mchango wake katika kuendeleza soka na ishara ya kutambua ushirikiano wa
kihistoria kati ya Castle Lager na FC Barcelona uliosainiwa hivi
karibuni huko Camp Nou Hispania. Wanaotazama ni Meneja Mauzo wa TBL
Kanda ya Kusini James Bokella (wa kwanza kulia) na Meneja Masoko wa TBL
Bi. Natalia Celani (wa pili kulia). Na kushoto ni Meneja wa Castle
Lager, Kabula Nshimo na Aggrey Marealle, Mkurugenzi wa Executive
Solutions washauri wa mahusiano wa TBL.
(PICHA NA IKULU)