Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, September 20, 2013

PICHA ZA HAKIMU ALIYECHOMWA KISU MAHAKAMANI KATIKA KESI YA BAISKELI HUKO SHINYANGA.



Baiskeli hiyo iliibiwa Agosti 1, mwaka huu katika eneo la Nguzo Nane katika Manispaa ya Shinyanga. Basikeli hiyo inadaiwa kuibwa na Daniel Makelezia mkazi wa Lubaga ambaye anafanya kazi ya ulinzi katika kampuni ambalo haijulikani.



Baada kesi hiyo kuendelea kusikilizwa katika mahakama hiyo Hakimu Nyangoha alitoa hukumu kwamba mshtakiwa akipatikana atahukumiwa gerezani kifungo cha miaka miwili jela.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa baada ya hukumu hiyo kutolewa mlalamikaji Emanuel Izengo miaka 28 ambaye ni mkazi wa maeneo ya Tambukaleri katika Manispaa ya Shinyanga aliyekuwa ameibiwa baiskeli aina ya Neria yenye thamani ya Sh150,000 alionekana kutoridhishwa na hukumu hiyo kutolewa bala mshtakiwa na mdhamini wake kutokuwapo mahakamani hapo.
Baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo mlalamikaji alitoa shukrani kwa kuwashika mikono wato wote waliokuwapo mahakamanai hapo na kutoka nje.


Lakini baada ya dakika 15 mlalamikaji Zengo alirudi mahakamani hapo na kudai kuwa ameleta risiti ya kumuonyesha hakimu thamani ya baiskeli yake, na alipoingia ndani ndipo kelele zilisikika za mshauri wa baraza la mahakama, Mery Wamba akisema 'njooni jamani hakimu amevamiwa anapigwa'


Watu walipofika katika ofisi kwa hakimu, walikuta amechomwa kisu katika shavu la upande wa kushoto huku akivuja damu nyingi sana, na mtuhumiwa huyo alikuwa anaendnelea kumchoma ndipo alipokamatwa.


Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga limethibitisha kutokea kwa tukio hilo mahakamani hapo na hakimu huyo alikimbizwa katika hospitali ya Mkoa wa Shinyanga ambako anapatiwa matibabu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages