Hitmaker wa Lava lava, Sarah Kaisi aka Shaa amesaini mkataba wa usamimizi wa miezi sita na kampuni ya Said Fela, ‘Mkubwa na Wanae’ akishirikiana na Babu Tale.
Akiongea na Bongo5, Fela amesema wameamua kumsimamia Shaa ili kumwezesha muziki wake uwafikie pia watu wa kawaida ambao kwa muda mrefu nyimbo zake za mwanzo zimekuwa zikiwabagua.
“Mimi ndio nilitoa hilo wazo, kwamba niliona Shaa anafanya kweli muziki mkubwa lakini kuna watu wanamiss vitu vyake hususan wale wa uchochoroni zaidi,” amesema Fela. “Nikamwambia Tale kama vipi tuongee na Master Jay, mimi nataka nioneshe kitu kwamba ndani ya miezi 6 atukabidhi sisi tufanye naye kazi ili tumlete kwa waswahili zaidi, Master J uzuri akatukubalia.
Japokuwa mkataba wenyewe ni mfupi, lakini tunaweza kuleta mapinduzi katika muziki wetu.”
“Tutakachomwambia afanye kile tunachokiona sisi cha kufanya kama anataka kufanya mduara afanye, kama anataka kufanya mchiriku afanye, kama tutaamua afanye ‘mkinda’ au ‘mkibiji’zote hizo itabidi Shaa afanye sababu kuna watu wanahitaji sauti ya Shaa kwenye hizo ngoma za Kiswahili.”
Fela amesema kwa kuanza Shaa ataachia wimbo uitwao Sugua Gaga uliotengenezwa na Shirko.
“Magaga ni yale yanayojitokeza kwenye kisigino, kukatikatika hivi,” amefafanua Fela.
Kwa upande wake Shaa ameiambia Bongo5 kuwa siku zote anapenda kufanya vitu tofauti na ndio maana ameingia mkataba huo na Fela. “Step iliyofuatia sasa ni kwamba nifanye vizuri kazi na Babu Tale na Fela ambao wao kwa pamoja wana kampuni yao ya Mkubwa na Wanaye. Nikaona sio vibaya nikiwajaribu na wao kwa pamoja sababu ni timu ambayo ni kali sana kwenye industry yetu,”amesema Shaa.
“Kwa kuanza tumesaini mkataba wa miezi 6. Ngoma ya kwanza kutoka inaitwa Sugua Gaga, lakini kuna ngoma kadhaa ambazo tumeshafanya ambazo na zenyewe zitafuata, kuna wimbo nimefanya na AT, umeandikwa na AT, kuna wimbo nimefanya na Shetta. Ni project ambayo naamini itanikeep busy sana na mashabiki wangu hawatanimiss kihivyo. Mwisho wa siku mimi kama Shaa napenda kufanya muziki ambao ni Afro-Pop Bongo Flava. Kwahiyo kwenye hii project vilevile sikutaka kukimbia sana huko, nikaona sio mbaya nikijaribu mandhari ya Mchiriku, Taarab, ambao mimi naamini bado ni Afro-Pop lakini kwajinsi nitakavyoifanya mimi ndio itakuwa KiShaa zaidi, kiAfri-Pop zaidi. Kwahiyo huu Sugua Gaga ni design hiyo,ni mchiriku zaidi.
Shaa amesema tayari ameshafanya nyimbo na watayarishaji kama Marco Chali, Manecky na Shirko.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Wednesday, October 9, 2013
Home
Unlabelled
SHAA ASAINI MKATABA NA SAID FELA AKISHIRIKIANA NA BABU TALE
SHAA ASAINI MKATABA NA SAID FELA AKISHIRIKIANA NA BABU TALE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment