Dar es Salaam. Mtanzania Stephen Ongolo
anayekabiliwa na madai ya kutishia kutoa siri za mke wa Rais Jacob Zuma,
Nompumelelo Ntuli (MaNtuli), huenda akarudishwa nchini na kuzuiwa
kuitembelea Afrika Kusini milele.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Tawi la
Uchunguzi wa Kesi, katika Jimbo la Kwa Zulu-Natal, Brigedia Clifford
Marion, wakati kesi ya Ongolo ilipokuwa ikisikilizwa katika Mahakama ya
Camperdown, jijini Durban.
Ilielezwa kuwa, Ongolo si raia wa Afrika
Kusini na kwamba alirudi nchini humo Januari 19 mwaka huu baada ya
kurejea kutoka katika mizunguko yake katika nchi kadhaa za Afrika
zikiwamo, Tanzania, Malawi, Msumbiji na Ethiopia.
Ilielezwa kuwa visa yake inamalizika Februari 18 mwaka huu.
“Atarudi nchini mwake Tanzania na hatarudi tena Afrika Kusini,” alisema Marion.
Chanzo chetu cha habari kilichohudhuria
kesi hiyo, kilisema Brigedia Marion alihojiwa kuhusu taarifa za mashtaka
dhidi ya Mtanzania huyo ambapo alitoa ushahidi kuwa Ongolo amekuwa
akituma ujumbe mfupi kwenye simu ya MaNtuli, akimtishia kuwa atatoa siri
kuhusu uhalali wa mtoto wake (MaNtuli).
Inadaiwa kuwa Ongolo katika ujumbe wake alidai kuwa mtoto mmoja wa MaNtuli si wa Rais Zuma.
Kabla ya kukamatwa, Ongolo alikwenda
katika vyombo vya habari kadhaa vya nchini humo na kudai kuwa, anafahamu
siri nzito kati ya MaNtuli na Phinda Thomo, aliyekuwa mlinzi wa
MaNtuli.
Thomo, alikutwa amejiua mwaka 2009
bafuni kwake, lakini Ongolo anadai kuwa Thomo hakuuawa na badala yake,
kifo chake kilipangwa kutokana na uhusiano wa siri kati yake na MaNtuli.
Mashtaka ya kutishiwa kuvujisha siri
zake, yalitolewa na MaNtuli ambaye alidai kuwa Ongolo amekuwa
akimlazimisha kumkutanisha kibiashara na Rais Zuma.
Brigedia Marion alitoa ushuhuda
mahakamani na kuiomba mahakama kukataa kutoa dhamana kwa Ongolo ambaye
alikamatwa mwishoni mwa Januari mwaka huu.
“Tofauti na inavyoandikwa kwenye
magazeti, Ongolo alikamatwa baada ya kufika ofisini kwangu akija
kulalamika kuwa kuna kesi ya wizi na uvamizi kwenye nyumba ya dada yake
ambayo inasimamiwa vibaya,” alisema Brigedia huyo.
Alisema, Ongolo alipofika ofisini hapo
alijitambulisha kama Stephen Ongolo lakini baadaye alibainika kama
Stephen John Masunga ndipo Marion akalikumbuka jina kwani MaNtuli
alikuwa ameshawasilisha mashtaka hayo polisi.
“Kukamatwa kwake ilikuwa ni bahati.
Nilipoona jina ni lilelile, nikaangalia namba ya simu niliyopewa na
MaNtuli na kuanza kuipiga na simu ya Ongolo ikaita na hapohapo nikamweka
chini ya ulinzi,” alisema Marion.
Ilidaiwa kuwa baada ya Ongolo kukamatwa,
simu yake na hati ya kusafiria vilichukuliwa na alipotakiwa kumpigia
simu wakili wake, hakufanya hivyo na badala yake alimpigia simu
mwandishi wa habari wa gazeti la Sunday Independent, Nathi Olifant.
Marion alisema, alikusanya ujumbe mfupi
kutoka kwenye simu za Ongolo na MaNtuli na kubaini kuwa wawili hao
waliwahi kukutana mwaka 2010.
Source: Mwananchi
Post Top Ad
Your Ad Spot
Friday, February 7, 2014
Home
EVENTS
GOSSIP
WHAT
SOMA STORI HII YA MTANZANIA ANAYETAKA KUVUJISHA SIRI ZA MKE WA RAIS JOCOB ZUMA WA SOUTH AFRICA.
SOMA STORI HII YA MTANZANIA ANAYETAKA KUVUJISHA SIRI ZA MKE WA RAIS JOCOB ZUMA WA SOUTH AFRICA.
Tags
EVENTS#
GOSSIP#
WHAT#
Share This
About DARVEL LAMAR BLOG
WHAT
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment