Katika
hali isiyokuwa ya kawaida na kushtua Msanii Manaiki Sanga a.k.a The Don
ameibuka na kumuumbua vibaya msanii mwenzake Diana Kimario ambae siku
za hivi karibuni amekuwa akijitangaza kama yeye ni bikra yani hajawahi
kuguswa na mwanaume kwa kushiriki tendo la ndoa.
Jambo
hilo limepingwa vikali na Manaiki ambae anadai ameishi na Diana kama
mkewe zaidi ya mwaka na nusu huku Mamaake Diana anaeishi Manzese akiwa
shahidi namba mjoa.
Akiongea
na paparazi Tanzania Manaiki Sanga alisema" Huu ni uongo uliokithiri
huyu demu amewadanganya watanzania yani anasema yeye bikra? Au bikra ya
wapi huenda sijaelewa mie?
Lakini
kama suala la mapenzi ya kawaida mimi nathibitisha kuwa hana ubikra
wowote amewahi kuwa mke wangu zaidi ya mwaka mmoja na ilikuwa nimuoe
kabisa lakini nilikuja kuchemka mwenyewe" Alisema Manaiki.
Aidha
mtandao huu ulimtafuta Diana ili kujibu hoja ya Manaiki Sanga lakini
kwa bahati mbaya hakuweza kupatikana hadi habari hii inaruka hewani na
kuwafikia wasomaji wetu makini.
No comments:
Post a Comment