Anaitwa Rob O’Neill, 38, aliyewahi kufanya mission za kijeshi zaidi ya 400.
Baba yake, Tom O’Neill anasema: “Watu wanauliza kama tunaogopa kwamba ISIS watakuja na kututeka kwasababu Rob anafahamika sasa. Nasema nitachora target kubwa kwenye mlango wangu wa mbele na kusema ‘njooni mtuteke’.
O’Neill mwenyewe alipongezwa na rais Barack Obama kwa kumuua bin Laden kwa risasi tatu juu ya paji lake la uso wakati wanajeshi wa Marekani waliposhambulia kambi yake huko Abbottabad, May 2, 2011.
O’Neill amekubali kufanyiwa mahojiano exclusive na kituo cha Fox baadaye mwezi huu.
Mission zake tatu alizozifanya zimetumika kwenye filamu za action za Hollywood. Alikuwa mwanajeshi aliyeongoza wenzie huko kuokoa meli ya Maersk Alabama, iliyokuwa imetekwa na maharamia wa Somalia ambapo operesheni hiyo ilizaa filamu ya Captain Phillips.
Alisaidia pia kuokolewa kwa Marcus Luttrell, mtu aliyeishi kusimua mpango uliofeli wa kumkamata kiongozi wa Taliban na kuzaliwa kwa filamu ‘Lone Survivor.’
Na pia alikuwa mtu aliyemuua Bin Laden kwenye Zero Dark Thirty.
No comments:
Post a Comment