Co-Starring wa Empire, Taraji P.Henson maarufu kwa jina la Cookie analotumia kwenye series hiyo, ameshare na followers wa Twitter tarehe ya kuanza kwa msimu wa pili ambayo ni September 23, 2015.
Hello! September 23 #Empire season ✌️ https://t.co/NWr7SmWk8a
— Taraji P. Henson (@TherealTaraji) May 29, 2015
Miongoni mwa mastaa waliotangazwa kuwa wataonekana katika msimu wa pili ni pamoja na mchekeshaji Chris Rock, muimbaji Alicia Keys na Lenny Kravitz, kwa mujibu wa mtandao wa AccessHollywood.Kutoka kushoto ni Hakeem, Jamal, Cookie na Lucious
Msimu mpya wa show hiyo unatarajiwa kuwa na episode 18 kutoka 12 zilizokuwepo msimu uliopita.
Series hiyo imekuwa gumzo kwa muda mfupi tu toka ilipozinduliwa January 7, 2015, si tu Marekani bali hata sehemu nyingi za dunia.
Empire imechezwa na Lucious (Terrence Howard) anayeigiza kama mmiliki wa label ya muziki inayoitwa Empire, akiwa na watoto wake watatu Adre (Trai Byeres), Jamal (Jussie Smollett) ambaye ni shoga lakini anauwezo mkubwa sana wa kuimba, na wa mwisho anaitwa Hakeem (Bryshere Gray) ambaye ni rapper. Yupo pia mke wa Lucious, Cookie ambaye ameonekana kuwa kivutio cha wengi katika msimu uliopita.
Ingia hapa kuifahamu zaidi Empire.
No comments:
Post a Comment