Jumatatu usiku (July 22) Beyonce alikuwa na show huko Montreal, Canada wakati anaimba wimbo wake wa ‘Hallo’ ghafla si nywele zake zikanaswa na feni iliyokuwa nyuma yake jukwaani hapo, nina uhakika kwa msanii mwingine angeweza hata kupoteza mwelekeo na huenda ingemharibia show, lakini uzoefu na kujiamini vilimsaidia Bey mama wa mtoto mmoja (Blue Ivy) ambaye hakutetereka na aliendelea kuimba bila hata kupoteza mstari wala kutoka nje ya beat (Ki professional zaidi). Bey alisimama kwa muda huku wasaidizi wake wakijaribu kukata sehemu ndogo ya nywele zake na mkasi ili aweze kuwa huru na kuendelea na show. Zoezi lilifanikiwa na kipenzi cha Jigga aliendeleza makamuzi.
Baada ya show hiyo Queen Bey (31) aliwaandikia mashabiki wake kile kilichotokea lakini katika hali ya utani zaidi. Kama ilivyokawaida yake Bey hupenda kuandika kwa mkono mkono na hiki ndicho alichoandika na kuki post Instagram “Gravity can’t begiiiiin to pull me out of the fan again. I felt my hair was yankiiiin from the fan that’s always hatiiiiin. Virgin remy and Malaysiiiiiaaaaaan. Haaaaaa, I got snatched “2 snaps.” Goodnight,”.
Tazama video ya tukio hilo