Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania, Yanga FC watacheza na Azam FC kesho kutwa (Jumamosi) kwenye mechi ya Ngao ya jamii kuashiria uzinduzi wa msimu mpya wa ligi 2013/2014.
Mechi hiyo inayotarajiwa kuwa kivutio kwa wapenzi wa mpira wa miguu nchini itachezwa kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10.30 jioni ambapo mshindi atakabidhiwa ngao.
Iwapo dakika 90 za mechi hiyo hazitatoa mshindi, timu hizo zitatenganishwa kwa mikwaju ya penalti huku asilimia 10 ya mapato ya mechi hiyo yakienda kwa kituo cha kulelea watoto cha SOS.
Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 7,000 kwa viti vya rangi ya kijani na bluu wakati viti vya rangi ya chungwa ni Sh10,000. Watakaiongia viti vya VIP C watalipa Sh15,000, viti vya VIP B ni Sh20,000 wakati VIP A watalipa Sh30,000.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Thursday, August 15, 2013
YANGA FC NA AZAM FC KUVAANA JUMAMOSI HII, NGAO YA JAMII
Tags
SPORTS#
Share This
About DARVEL LAMAR BLOG
SPORTS
Labels:
SPORTS
Post Top Ad
Your Ad Spot
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.