Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, October 15, 2013

MWANAMKE HUYU AENDESHA GARI RICHA YA ONYO,SHERIA NA VITISHO VYA NCHI YA SAUDI ARABIA, WANAWAKE KUTORUHUSIWA NCHINI HUMO.

Ukraine Protest
Nakuletea hii stori kutoka Saudi Arabia ikiwa ni nchi pekee duniani iliyovunja rekodi kwa Wanawake kutoruhusiwa kuendesha magari, ishu ambayo imekua ikipingwa na nchi mbalimbali na hata baadhi ya Wasaudia wenyewe.
Pamoja na kwamba Wanawake hawatakiwi kuendesha magari, kwa mujibu wa MEMRI TV Wanawake wanaruhusiwa kufanya kazi nyingine au kuonekana vyuoni, kufanya kazi kwenye Hospitali, Mainjinia na kufanyaa biashara pia.
Saudia 2
Waziri anaehusika na maswala ya sheria Saudi Arabia anasema ‘ hii imetokana na jamii na utamaduni wake.. kama jamii ya Wasaudia itakubali Wanawake waendeshe magari ni sawa lakini kama hawataki pia ni uamuzi wao’
Unaambiwa kuna video imevuja ikimuonyesha mwanamke akiwa anaendesha gari hukohuko Saudi Arabia ambapo magari kadhaa yaliyompita na kugundua kwamba ni Mwanamke, waliokuwemo ndani ya hayo magari walimpungia na wengine kumpiga picha, baadhi ya Wanaume waliompita kwa pembeni walionekana kupunguza speed na kumpa alama ya dole wakiashiria kusupport alichokifanya huyu Mwanamke.
Hii imekua stori kwa sababu ni mara chache SANA kuona Mwanamke anaendesha gari nchini Saudia ndio maana yeyote atakaeonekana lazima achukue headlines.
1
Akiwa kwenye usukani mwenyewe…
2
Akipewa dole la hongera kutoka kwenye gari lililompita.
3
Hongera kutoka kwa gari jingine

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages